KING JAMES BIBLETafuta

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™

Zaburi 101

Zote · ZaburiTafuta

1Nitaimba juu ya upendo wako na haki yako; kwako wewe, Ee Bwana , nitaimba sifa.

2Nitazingatia kuishi maisha yasiyo na lawama: utakuja kwangu lini? Nitatembea nyumbani mwangu kwa moyo usio na lawama.

3Sitaweka mbele ya macho yangu kitu kiovu. Ninayachukia matendo ya watu wasio na imani; hawatashikamana nami.

4Moyo wa ukaidi utakuwa mbali nami; nitajitenga na kila ubaya.

5Kila amsingiziaye jirani yake kwa siri, huyo nitamnyamazisha; mwenye macho ya dharau na moyo wa kiburi huyo sitamvumilia.

6Macho yangu yatawaelekea waaminifu katika nchi, ili waweze kuishi pamoja nami; yeye ambaye moyo wake hauna lawama atanitumikia.

7Mdanganyifu hatakaa nyumbani mwangu, yeye asemaye kwa uongo hatasimama mbele yangu.

8Kila asubuhi nitawanyamazisha waovu wote katika nchi; nitamkatilia mbali kila mtenda mabaya kutoka mji wa Bwana .

Sources and attribution