KING JAMES BIBLETafuta

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™

Zaburi 121

Zote · ZaburiTafuta

1Nayainua macho yangu nitazame vilima, msaada wangu utatoka wapi?

2Msaada wangu hutoka kwa Bwana , Muumba wa mbingu na dunia.

3Hatauacha mguu wako uteleze, yeye akulindaye hatasinzia,

4hakika, yeye alindaye Israeli hatasinzia wala hatalala usingizi.

5Bwana anakulinda, Bwana ni uvuli wako mkono wako wa kuume,

6jua halitakudhuru mchana, wala mwezi wakati wa usiku.

7Bwana atakukinga na madhara yote, atayalinda maisha yako,

8Bwana atakulinda unapoingia na unapotoka, tangu sasa na hata milele.

Sources and attribution