KING JAMES BIBLETafuta

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™

Zaburi 136

Zote · ZaburiTafuta

1Mshukuruni Bwana , kwa kuwa ni mwema. Fadhili zake zadumu milele .

2Mshukuruni Mungu wa miungu. Fadhili zake zadumu milele .

3Mshukuruni Bwana wa mabwana: Fadhili zake zadumu milele .

4Kwake yeye pekee atendaye maajabu makuu, Fadhili zake zadumu milele .

5Ambaye kwa ufahamu wake aliziumba mbingu, Fadhili zake zadumu milele .

6Ambaye aliitandaza dunia juu ya maji, Fadhili zake zadumu milele .

7Ambaye aliumba mianga mikubwa, Fadhili zake zadumu milele .

8Jua litawale mchana, Fadhili zake zadumu milele .

9Mwezi na nyota vitawale usiku, Fadhili zake zadumu milele .

10Kwake yeye aliyemuua mzaliwa wa kwanza wa Misri, Fadhili zake zadumu milele .

11Na kuwatoa Israeli katikati yao, Fadhili zake zadumu milele .

12Kwa mkono wenye nguvu ulionyooshwa, Fadhili zake zadumu milele .

13Kwake yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu, Fadhili zake zadumu milele .

14Na kuwapitisha Israeli katikati yake, Fadhili zake zadumu milele .

15Lakini alimfagia Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu, Fadhili zake zadumu milele .

16Kwake yeye aliyewaongoza watu wake katika jangwa, Fadhili zake zadumu milele .

17Ambaye aliwapiga wafalme wenye nguvu, Fadhili zake zadumu milele .

18Naye aliwaua wafalme wenye nguvu, Fadhili zake zadumu milele .

19Sihoni mfalme wa Waamori, Fadhili zake zadumu milele .

20Ogu mfalme wa Bashani, Fadhili zake zadumu milele .

21Akatoa nchi yao kuwa urithi, Fadhili zake zadumu milele .

22Urithi kwa Israeli mtumishi wake, Fadhili zake zadumu milele .

23Aliyetukumbuka katika unyonge wetu, Fadhili zake zadumu milele .

24Alituweka huru toka adui zetu, Fadhili zake zadumu milele .

25Ambaye humpa chakula kila kiumbe. Fadhili zake zadumu milele .

26Mshukuruni Mungu wa mbinguni, Fadhili zake zadumu milele .

Sources and attribution