KING JAMES BIBLETafuta

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™

Zaburi 23

Zote · ZaburiTafuta

1Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu.

2Hunilaza katika malisho ya majani mabichi, kando ya maji matulivu huniongoza,

3hunihuisha nafsi yangu. Huniongoza katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.

4Hata kama nikipita katikati ya bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya, kwa maana wewe upo pamoja nami; fimbo yako na mkongojo wako vyanifariji.

5Waandaa meza mbele yangu machoni pa adui zangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, kikombe changu kinafurika.

6Hakika wema na upendo vitanifuata siku zote za maisha yangu, nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele.

Sources and attribution