KING JAMES BIBLETafuta

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™

Zaburi 3

Zote · ZaburiTafuta

1Ee Bwana , tazama adui zangu walivyo wengi! Ni wengi kiasi gani wanaoinuka dhidi yangu!

2Wengi wanasema juu yangu, “Mungu hatamwokoa.”

3Lakini wewe, Ee Bwana , ni ngao pande zote; umeniwekea utukufu na kuinua kichwa changu.

4Ninamlilia Bwana kwa sauti kuu, naye ananijibu kutoka mlima wake mtakatifu.

5Ninajilaza na kupata usingizi; naamka tena, kwa maana Bwana hunitegemeza.

6Sitaogopa makumi elfu ya adui, wanaojipanga dhidi yangu kila upande.

7Ee Bwana , amka! Niokoe, Ee Mungu wangu! Wapige adui zangu wote kwenye taya, vunja meno ya waovu.

8Kwa maana wokovu watoka kwa Bwana . Baraka yako na iwe juu ya watu wako.

Sources and attribution