KING JAMES BIBLETafuta

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™

Zaburi 67

Zote · ZaburiTafuta

1Mungu aturehemu na kutubariki, na kutuangazia nuru za uso wake,

2ili njia zako zijulikane duniani, wokovu wako katikati ya mataifa yote.

3Ee Mungu, mataifa na wakusifu, mataifa yote na wakusifu.

4Mataifa yote wafurahi na kuimba kwa shangwe, kwa kuwa unatawala watu kwa haki na kuongoza mataifa ya dunia.

5Ee Mungu, mataifa na wakusifu, mataifa yote na wakusifu.

6Ndipo nchi itatoa mazao yake, naye Mungu, Mungu wetu, atatubariki.

7Mungu atatubariki na miisho yote ya dunia itamcha yeye.

Sources and attribution