KING JAMES BIBLETafuta

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™

Zaburi 93

Zote · ZaburiTafuta

1Bwana anatawala, amejivika utukufu; Bwana amejivika utukufu tena amejivika nguvu. Dunia imewekwa imara, haitaondoshwa.

2Kiti chako cha enzi kimekuwa thabiti tangu zamani; wewe umekuwako tangu milele.

3Bahari zimeinua, Ee Bwana , bahari zimeinua sauti zake; bahari zimeinua sauti za mawimbi yake.

4Yeye ni mkuu kuliko ngurumo ya maji makuu, ni mkuu kuliko mawimbi ya bahari: Bwana aishiye juu sana ni mkuu.

5Ee Bwana , sheria zako ni imara; utakatifu umepamba nyumba yako pasipo mwisho.

Sources and attribution