Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
Zaburi 99
1Bwana anatawala, mataifa na yatetemeke; anakalia kiti cha enzi katikati ya makerubi, dunia na itikisike.
2Bwana ni mkuu katika Sayuni; ametukuzwa juu ya mataifa yote.
3Wanalisifu jina lako ambalo ni kuu na la kuogopwa: yeye ni mtakatifu!
4Mfalme ni mwenye nguvu na hupenda haki, wewe umethibitisha adili; katika Yakobo umefanya yaliyo haki na sawa.
5Mtukuzeni Bwana Mungu wetu, na mkaabudu katika mahali pa kuwekea miguu yake; yeye ni mtakatifu.
6Mose na Aroni walikuwa miongoni mwa makuhani wake, Samweli alikuwa miongoni mwa walioliitia jina lake; walimwita Bwana , naye aliwajibu.
7Alizungumza nao kutoka nguzo ya wingu; walizishika sheria zake na amri alizowapa.
8Ee Bwana , wetu, ndiwe uliyewajibu, kwa Israeli ulikuwa Mungu mwenye kusamehe, ingawa uliadhibu matendo yao mabaya.
9Mtukuzeni Bwana Mungu wetu, mwabuduni kwenye mlima wake mtakatifu, kwa maana Bwana Mungu wetu ni mtakatifu.