KING JAMES BIBLETafuta

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™

Zaburi 12

Zote · ZaburiTafuta

1Bwana tusaidie, kwa kuwa wacha Mungu wametoweka; waaminifu wametoweka miongoni mwa wanadamu.

2Kila mmoja humwambia jirani yake uongo; midomo yao ya hila huzungumza kwa udanganyifu.

3Bwana na akatilie mbali midomo yote ya hila na kila ulimi uliojaa majivuno,

4ule unaosema, “Kwa ndimi zetu tutashinda; midomo ni mali yetu, bwana wetu ni nani?”

5“Kwa sababu ya uonevu wa wanyonge na kulia kwa uchungu kwa wahitaji, nitainuka sasa,” asema Bwana . “Nitawalinda kutokana na wale wenye nia mbaya juu yao.”

6Maneno ya Bwana ni safi, kama fedha iliyosafishwa katika tanuru, iliyosafishwa mara saba.

7Ee Bwana , utatuweka salama na kutulinda na kizazi hiki milele.

8Watu waovu huenda wakiringa kila mahali wakati ambapo yule aliye mbaya sana ndiye anayeheshimiwa miongoni mwa watu.

Sources and attribution