KING JAMES BIBLETafuta

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™

Zaburi 13

Zote · ZaburiTafuta

1Mpaka lini, Ee Bwana ? Je, utanisahau milele? Utanificha uso wako mpaka lini?

2Nitapambana na mawazo yangu mpaka lini, na kila siku kuwa na majonzi moyoni mwangu? Adui zangu watanishinda mpaka lini?

3Nitazame, unijibu, Ee Bwana Mungu wangu. Yatie nuru macho yangu, ama sivyo nitalala usingizi wa mauti.

4Adui yangu atasema, “Nimemshinda,” nao adui zangu watashangilia nitakapoanguka.

5Lakini ninategemea upendo wako usiokoma; moyo wangu unashangilia katika wokovu wako.

6Nitamwimbia Bwana , kwa kuwa amekuwa mwema kwangu.

Sources and attribution