Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
Zaburi 131
1Moyo wangu hauna kiburi, Ee Bwana , macho yangu hayajivuni; sijishughulishi na mambo makuu kunizidi wala mambo ya ajabu mno kwangu.
2Lakini nimetuliza na kunyamazisha nafsi yangu; kama mtoto aliyeachishwa kunyonya na mama yake, kama mtoto aliyeachishwa kunyonya ndivyo ilivyo nafsi iliyoko ndani yangu.
3Ee Israeli, mtumaini Bwana tangu sasa na hata milele.