Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
Zaburi 130
1Kutoka vilindini ninakulilia, Ee Bwana .
2Ee Bwana , sikia sauti yangu. Masikio yako na yawe masikivu kwa kilio changu unihurumie.
3Kama wewe, Ee Bwana , ungeweka kumbukumbu ya dhambi, Ee Bwana, ni nani angeliweza kusimama?
4Lakini kwako kuna msamaha, kwa hiyo wewe unaogopwa.
5Namngojea Bwana , nafsi yangu inangojea, katika neno lake naweka tumaini langu.
6Nafsi yangu inamngojea Bwana kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi, naam, kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi.
7Ee Israeli, mtumaini Bwana , maana kwa Bwana kuna upendo usiokoma, na kwake kuna ukombozi kamili.
8Yeye mwenyewe ataikomboa Israeli kutoka dhambi zao zote.