KING JAMES BIBLETafuta

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™

Zaburi 129

Zote · ZaburiTafuta

1Wamenionea mno tangu ujana wangu; Israeli na aseme sasa:

2wamenionea mno tangu ujana wangu, lakini bado hawajanishinda.

3Wakulima wamelima mgongo wangu, na kufanya mifereji yao mirefu.

4Lakini Bwana ni mwenye haki; amenifungua toka kamba za waovu.

5Wale wote waichukiao Sayuni na warudishwe nyuma kwa aibu.

6Wawe kama majani juu ya paa, ambayo hunyauka kabla hayajakua;

7kwa hayo mvunaji hawezi kujaza vitanga vyake, wala akusanyaye kujaza mikono yake.

8Wale wapitao karibu na wasiseme, “Baraka ya Bwana iwe juu yako; tunakubariki katika jina la Bwana .”

Sources and attribution