KING JAMES BIBLETafuta

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™

Zaburi 87

Zote · ZaburiTafuta

1Ameuweka msingi wake katika mlima mtakatifu;

2Bwana anayapenda malango ya Sayuni kuliko makao yote ya Yakobo.

3Mambo matukufu yanasemwa juu yako, ee mji wa Mungu:

4“Nitaweka kumbukumbu ya Rahabu na Babeli miongoni mwa wale wanaonikubali mimi: Ufilisti pia na Tiro, pamoja na Kushi, nami nitasema, ‘Huyu alizaliwa Sayuni.’ ”

5Kuhusu Sayuni itasemwa hivi, “Huyu na yule walizaliwa humo, naye Aliye Juu Sana mwenyewe atamwimarisha.”

6Bwana ataandika katika orodha ya mataifa: “Huyu alizaliwa Sayuni.”

7Watakapokuwa wanapiga vinanda wataimba, “Chemchemi zangu zote ziko kwako.”

Sources and attribution